Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yoshua
Hesabu 13 : 8
8 Katika kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni
1 Mambo ya Nyakati 7 : 27
27 ⑦ na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.
Kutoka 24 : 13
13 Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu.
Kutoka 32 : 17
17 Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, Kuna kelele ya vita kambini.
Kutoka 33 : 11
11 Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata kambini; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.
Hesabu 11 : 28
28 Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa tangu ujana wake, akajibu akasema, Ee bwana wangu Musa, uwakataze.
Hesabu 13 : 8
8 Katika kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni
Hesabu 14 : 10
10 Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.
Hesabu 14 : 30
30 hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliapa kwa kuinua mkono wangu, kwamba nitawafanyia makao humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.
Hesabu 14 : 38
38 ⑥ Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.
Hesabu 32 : 12
12 ⑩ ila Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni; kwa kuwa wao wamemwandama BWANA kwa moyo wote.
Hesabu 27 : 23
23 kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa.
Kumbukumbu la Torati 1 : 38
38 Yoshua mwana wa Nuni asimamaye mbele yako ndiye atakayeingia; mtie moyo; kwa kuwa yeye atawarithisha Israeli.
Kumbukumbu la Torati 3 : 28
28 ② Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na nguvu, umtie na nguvu; kwani ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, na nchi utakayoiona atawarithisha yeye.
Kumbukumbu la Torati 31 : 3
3 ④ BWANA Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama BWANA alivyonena.
Kumbukumbu la Torati 31 : 7
7 ⑧ Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi BWANA aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha.
Kumbukumbu la Torati 31 : 23
23 Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe.
Leave a Reply