Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yesu, Kristo
Mathayo 1 : 17
17 Basi vizazi vyote tangu Abrahamu hadi Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hadi ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hadi Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Luka 3 : 38
38 ⑰ wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.
Luka 1 : 38
38 Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
Luka 1 : 56
56 Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.
Luka 1 : 55
55 ③ Kama alivyowaambia baba zetu, Abrahamu na uzao wake hata milele.
Mathayo 1 : 25
25 asimjue kamwe hadi alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.
Luka 2 : 7
7 ⑲ akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Luka 2 : 20
20 Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.
Mathayo 2 : 12
12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
Luka 2 : 21
21 Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
Luka 2 : 38
38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
Mathayo 2 : 23
23 ① akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazareti.
Leave a Reply