Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yerusalemu
Zaburi 122 : 3 – 5
3 Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana,
4 Huko ndiko wapandako kabila, makabila ya BWANA; Kama ulivyowaamuru Waisraeli, Walishukuru jina la BWANA.
5 Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya ukoo wa Daudi.
Zaburi 122 : 6
6 Uombeeni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;
Zaburi 125 : 2
2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.
Zaburi 48 : 2
2 Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni, kule upande wa kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.
Isaya 62 : 3
3 Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.
Ezra 10 : 9
9 ⑫ Ndipo wanaume wote wa Yuda na Benyamini wakakusanyika katika muda wa siku tatu; ulikuwa mwezi wa tisa, siku ya ishirini ya mwezi; na watu wote wakaketi katika uwanja, mbele ya nyumba ya Mungu, wakitetemeka kwa sababu ya neno hilo, na kwa sababu ya mvua kubwa.
Yeremia 32 : 31
31 Kwa kuwa mji huu umekuwa sababu ya kunitia hasira, na sababu ya ghadhabu yangu, tangu siku ile walipoujenga hata siku hii ya leo; ili niuondoe usiwe mbele za uso wangu;
1 Wafalme 15 : 4
4 ⑤ Lakini kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu;
Leave a Reply