Biblia inasema nini kuhusu wenye nia mbili – Mistari yote ya Biblia kuhusu wenye nia mbili

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia wenye nia mbili

Yakobo 1 : 6 – 8
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.

Yakobo 4 : 8
8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

Yakobo 1 : 8
8 Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.

Yakobo 1 : 22 – 25
22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

1 Petro 5 : 8
8 ⑲ Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Yakobo 4 : 7
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

2 Wakorintho 7 : 1
1 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu kutoka kwa uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.

1 Petro 4 : 12 – 13
12 ④ Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.
13 ⑤ Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili pia katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.

Yakobo 1 : 22
22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

Yakobo 4 : 3
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

Yakobo 1 : 1 – 27
1 Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mawili waliotawanyika; salamu.
2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
5 Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.
9 Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa;
10 bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana atatoweka kama ua la majani.
11 Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.
12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
13 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
16 Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.
17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
18 Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.
19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
20 kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.
21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.
27 Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

2 Wakorintho 11 : 3
3 ⑪ Lakini nahofu; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

1 Yohana 3 : 22
22 na lolote tuombalo, tunalipokea kwake, kwa kuwa tunazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

Yakobo 2 : 8
8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.

2 Wakorintho 10 : 5
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;

Warumi 6 : 22
22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.

Mathayo 27 : 1 – 66
1 Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa mtawala.
3 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nilikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.
4 Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.
5 Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.
6 Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni fedha ya damu.
7 Wakafanya shauri, wakavitumia kwa kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.
8 Kwa hiyo shamba lile huitwa shamba la damu hata leo.
9 Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima;
10 wakavitumia kwa kununua shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.
11 Naye Yesu akasimama mbele ya mtawala; mtawala akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wasema.
12 Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno.
13 Ndipo Pilato akamwambia, Husikii ni mambo mangapi wanayoshuhudia juu yako?
14 Asimjibu hata neno moja, hata mtawala akastaajabu sana.
15 Basi wakati wa sikukuu, mtawala desturi yake huwafungulia mkutano mfungwa mmoja waliyemtaka.
16 Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba.
17 Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?
18 Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa ajili ya husuda.
19 Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.
20 Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.
21 Basi mtawala akajibu, akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi kati ya hawa wawili? Wakasema, Baraba.
22 Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulubiwe.
23 Akasema, Kwa nini? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulubiwe.
24 Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lolote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.
25 Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.
26 Ndipo akawafungulia Baraba; na baada ya kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa ili asulubiwe.
27 ① Ndipo askari wa mtawala wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio,[8] wakamkusanyikia kikosi kizima.
28 Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.
29 Wakasokota taji la miiba, wakaliweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kulia; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!
30 ② Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampigapiga kichwani.
31 ③ Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulubisha.
32 Walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.
33 Na walipofika mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la Kichwa,
34 ④ wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.
35 ⑤ Walipokwisha kumsulubisha, waligawana mavazi yake, kwa kupiga kura; [ili litimie neno lililonenwa na nabii, Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.]
36 Wakaketi, wakamlinda huko.
37 Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.
38 ⑥ Wakati uo huo wanyang’anyi wawili wakasulubiwa pamoja naye, mmoja katika mkono wake wa kulia, na mmoja katika mkono wake wa kushoto.
39 ⑦ Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema,
40 ⑧ Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.
41 Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.
42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
43 ⑩ Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.
44 Pia wale wanyang’anyi waliosulubiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.
45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hadi saa tisa.
46 ⑪ Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
47 Na baadhi yao waliokuweko, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya.
48 ⑫ Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha.
49 Wale wengine wakasema, Acha; na tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.
50 Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 ⑬ Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hadi chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
53 ⑭ nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
54 Basi yule afisa, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la ardhi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
55 ⑮ Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, hao ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia.
56 ⑯ Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.
57 ⑰ Na ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;⑱
58 mtu huyu alimwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe.
59 Yusufu akautwaa mwili, akauzongazonga katika sanda ya kitani safi,
60 ⑲ akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
61 Na pale walikuwapo Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, wameketi kulielekea kaburi.
62 Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato,
63 ⑳ wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa angali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.
64 Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hadi siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.
65 Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo.
66 Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe mhuri, pamoja na kuwaweka wale askari walinzi.

Mathayo 5 : 5
5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.

Warumi 8 : 28
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Zaburi 103 : 1 – 22
1 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.
2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 ⑤ Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
4 Aukomboa uhai wako kutoka kwa kaburi, Akutia taji la fadhili na rehema,
5 Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;
6 BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa.
7 Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake.
8 ⑥ BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
9 ⑦ Yeye hatashutumu daima, Wala hatashika hasira yake milele.
10 ⑧ Hakututenda kulingana na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
11 Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.
12 ⑩ Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 ⑪ Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.
14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.
15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo anavyostawi.
16 Maana upepo hupita juu yake, na kutoweka! Lisionekane mahali lilipokuwa tena.
17 ⑫ Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ni kwa vizazi vyote;
18 ⑬ Kwa wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.
19 ⑭ BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.
20 ⑮ Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
21 ⑯ Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.
22 Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *