Biblia inasema nini kuhusu Watoto – Mistari yote ya Biblia kuhusu Watoto

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Watoto

Mwanzo 15 : 5
5 Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

Mwanzo 21 : 2
2 Sara akapata mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.

Mwanzo 25 : 21
21 Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

Mwanzo 30 : 22
22 Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.

Mwanzo 30 : 24
24 Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine.

1 Samweli 1 : 20
20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume; akamwita Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.

Luka 1 : 13
13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana.

Ezekieli 16 : 6
6 Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nilikuambia, Ulipokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nilikuambia, Ulipokuwa katika damu yako, uwe hai.

Luka 2 : 7
7 ⑲ akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

Waamuzi 13 : 5
5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.

Waamuzi 13 : 7
7 lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hadi siku ya kufa kwake.

1 Samweli 1 : 28
28 kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.

Kumbukumbu la Torati 7 : 12
12 Na itakuwa, kwa sababu mnazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;

Kumbukumbu la Torati 7 : 14
14 Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mwanamume wala mwanamke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa kufugwa.

Ayubu 5 : 25
25 Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi, Na uzao wako utakuwa kama nyasi za nchi.

Zaburi 128 : 4
4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.

Zaburi 128 : 6
6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *