Biblia inasema nini kuhusu Wapelelezi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Wapelelezi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wapelelezi

Mwanzo 42 : 9
9 ④ Yusufu akazikumbuka zile ndoto alizowaotea. Akawaambia, Wapelelezi ninyi, mmekuja ili mwuone utupu wa nchi.

Hesabu 21 : 32
32 ⑫ Kisha Musa akatuma watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo.

Yoshua 2 : 1
1 Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Nendeni mkaitazame nchi hii, hasa Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.

1 Samweli 26 : 4
4 Basi Daudi akatuma wapelelezi, akapata habari ya hakika ya kwamba Sauli amefika.

2 Samweli 15 : 10
10 Lakini Absalomu akatuma wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anatawala huko Hebroni.

2 Samweli 17 : 17
17 ⑥ Basi Yonathani na Ahimaasi walikuwa wakikaa karibu na Enrogeli; na mjakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapa habari; ndipo wakamwambie mfalme Daudi; maana ilikuwa lazima wasionekane wakiingia mjini.

Luka 20 : 20
20 ⑧ Wakamviziavizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya mtawala. ⑩

Wagalatia 2 : 4
4 Bali kwa ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri; ambao waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *