Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wafungwa
Mwanzo 39 : 23
23 ⑧ Wala mkuu wa gereza hakufuatilia kazi liliyokuwa mikononi mwa Yusufu; kwa kuwa BWANA alikuwa pamoja naye. BWANA akayafanikisha yote aliyoyafanya.
Mwanzo 41 : 44
44 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.
Yeremia 38 : 28
28 ⑳ Basi Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi hadi siku ile Yerusalemu ulipotwaliwa.
Yeremia 39 : 14
14 wakatuma watu wakamwondoa Yeremia katika uwanda wa walinzi, wakamweka katika mikono ya Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ili ampeleke nyumbani kwake; basi akakaa pamoja na hao watu.
Mathayo 11 : 2
2 ⑰ Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,⑱
Mathayo 14 : 12
12 Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Marko 6 : 17
17 ⑲ Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo, ndugu yake, kwa kuwa amemwoa;
Luka 3 : 20
20 aliongeza na hili juu ya yote, alimfunga Yohana gerezani.
Mathayo 26 : 75
75 Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.
Marko 14 : 72
72 Na mara jogoo akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia.
Luka 22 : 71
71 Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.
Yohana 18 : 40
40 Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang’anyi.
Matendo 5 : 42
42 Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri Habari Njema za Yesu kwamba ni Kristo.
Matendo 12 : 19
19 Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwahoji wale walinzi, akaamuru wauawe. Kisha akateremka kutoka Yudea kwenda Kaisaria, akakaa huko.
Matendo 16 : 40
40 Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Lidia; na walipokwisha kuonana na ndugu wakawafariji, wakaenda zao.
Matendo 21 : 40
40 Basi, alipompa ruhusa, Paulo akasimama madarajani, akawapungia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania.
Matendo 16 : 40
40 Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Lidia; na walipokwisha kuonana na ndugu wakawafariji, wakaenda zao.
Waamuzi 16 : 21
21 Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
Leave a Reply