Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia vyombo vya muziki kanisani
Zaburi 150 : 1 – 6
1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 ① Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.
Zaburi 150 : 3 – 5
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
Waefeso 5 : 19
19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
Yakobo 5 : 13
13 Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Ufunuo 14 : 2 – 3
2 ⑯ Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;
3 ⑰ na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale elfu mia moja na arubaini na nne, walionunuliwa katika nchi.
Waefeso 5 : 15 – 25
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu.
17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
21 Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Ufunuo 5 : 8 – 14
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa maelfu na mamilioni,
12 ① wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13 ② Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nilivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwake Mwana-kondoo, hata milele na milele.
14 ③ Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
Zaburi 98 : 4 – 6
4 Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni sifa.
5 Mwimbieni BWANA sifa kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti tamu.
6 ⑲ Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.
Zaburi 150 : 3 – 4
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
Zaburi 18 : 49
49 Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.
1 Wakorintho 14 : 15
15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.
Zaburi 81 : 1 – 2
1 Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo.
2 Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.
Luka 15 : 21 – 25
21 Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena.
22 Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
23 mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi;
24 ⑲ kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwa shambani na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na nderemo.
Leave a Reply