Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Viwanda
Mwanzo 2 : 15
15 BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Kutoka 23 : 12
12 Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng’ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika.
Kumbukumbu la Torati 5 : 13
13 ⑤ Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
Kutoka 35 : 2
2 Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa BWANA; mtu yeyote atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo atauawa.
Mithali 10 : 5
5 Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
Mithali 12 : 11
11 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu.
Mithali 12 : 24
24 ⑥ Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.
Mithali 12 : 27
27 Mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Mithali 13 : 4
4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
Mithali 13 : 11
11 ⑭ Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.
Mithali 13 : 23
23 Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.
Mithali 14 : 4
4 Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi.
Mithali 14 : 23
23 Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.
Mithali 16 : 26
26 Nafsi yake mfanyakazi hujifanyia kazi; Maana kinywa chake humtia bidii.
Mithali 20 : 13
13 ⑩ Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.
Mithali 21 : 5
5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.
Mithali 22 : 29
29 Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.
Mithali 27 : 27
27 Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako.
Mithali 28 : 19
19 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
Mithali 30 : 28
28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
Mithali 31 : 27
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
Mhubiri 1 : 3
3 Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
Mhubiri 2 : 11
11 Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kufukuza upepo, wala faida hakuna chini ya jua.
Mhubiri 2 : 22
22 Kwa maana mtu hupata nini kwa kazi yake yote, na kwa juhudi ya moyo wake alivyojitahidi chini ya jua?
Mhubiri 9 : 10
10 Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Mhubiri 11 : 4
4 Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
Mhubiri 11 : 6
6 Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiulegeze mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.
Leave a Reply