Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uzia
2 Wafalme 14 : 21
21 Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia,[8] aliyekuwa mwenye umri wa miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa baba yake Amazia.
2 Wafalme 15 : 2
2 Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na miwili huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 1
1 Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 3
3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili; na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu.
2 Wafalme 14 : 22
22 Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 2
2 Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze.
2 Wafalme 15 : 3
3 Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, kama yote aliyoyafanya babaye Amazia.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 5
5 Akajitia nia amtafute Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na fahamu katika maono ya Mungu; na muda alipomtafuta BWANA, Mungu alimfanikisha.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 7
7 ① Mungu akamsaidia juu ya Wafilisti, na juu ya Waarabu waliokaa Gur-baali, na juu ya Wameuni.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 8
8 ② Na Waamoni wakampa Uzia zawadi; likaenea jina lake mpaka Misri; alipata nguvu nyingi.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 9
9 ③ Tena Uzia akaujengea Yerusalemu minara, penye Lango la Pembeni, na penye Lango la Bondeni, na ugeukapo ukuta, akaitia nguvu.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 10
10 ④ Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na ng’ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 15
15 Huko Yerusalemu akatengeneza mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu mastadi, iwekwe juu ya minara na juu ya buruji, ili kurusha mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 21
21 ⑪ Uzia mfalme akawa na ukoma hadi siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya BWANA; na Yothamu mwanawe alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme, akiwatawala watu wa nchi.
Leave a Reply